Kiswahili: Matangazo ya tarehe 2 Januari 2026 kwenye Kivu news today

Hii ni Kivu news today TV iki kutangaziya kutoka mashariki mwa DRC. Unaweza kutufuata kwenye baadhi ya  mitandao ya kijamii mukiwemo Youtube, Facebook, intagram, na X, pia kwenye internet www.kivunewstoday.com

1 Tuanzie habari zetu mjini Gomamakao makuu ya mkowani Kivu kaskazini, amabako meja Generali Sultani Makenga kamanda mkuu wa jeshi la ARC ajulisha makadazi wa chama AFC umuhimu kwao kujitowa na kuweka nguvu katika kazi wanayofanya lakini akiwaalika kuwa na umoja njia moja ya kushinda vita hivi.

 Ilikuwa katika mkutano wa mwisho wa mwaka ulio endeshwa mwa,zo ni mwa juma hii kwenyi ikulu ya liwali wa jimbo ya Kivu kaskazini

Katika hotuba yake meja generali Sultani Makenga alisisitiza makadazi hawa kuyazingatiya yale walio funzwa wakiweka mbele umoja na kupiganisha ubaguzi

2 Tukiwa bado katika  jiji la  Goma mashariki mwa DRC amabapo sikumoja imetosha ili watu warejeye kazini baada ya kusherekea mwaka mpya wa 2026. Hii ijumaa kazi tofauti ziliendeshwa kwa usawa na raiya wote wameshuhudiya kwamba sherehe za mwaka mpya zimepita kwa hali ya utulivu katika eneo zote za jijini Goma.

Raiya wa Goma wasema kuwa waridhishwa na namna jinsi sherehe zimeendeshwa kwa usalama lakini pia ongezeko kiucumi kwao  ambayo kulionekana tofauti na siku zingine

3 Na katika lengo la kuimarisha hali ya Usafi ndani ya jiji la Goma baada ya sherehe za mwaka mpya, meya makamu wa  Goma Desire Ngabo Kisuba aalika wakaaji kuendelea kuzingatiya kanuni za usafi na  kuepuka wao kuanguka katika makosa.

Alizungumza huvyo hii ijuma, siku moja baada ya sherehe za kuanza mwaka mpya. Desire Ngabo Kisuba asema kwamba uongozi hauwezi kuaciliya mtu yeyote ambaye atajaribu kuharibu sura ya usafi yam ji wa Goma

4 Na huko wilayani Masisi, watu sita kufariki na  wengine wengi kujeruhiwa vikali hayo ndiyo matokeo ya shambulizi ya ndege ya vita aina Sukoi ilio rusha  bomu katika raiya wa masisi centre  hii ijumaa tarehe mbili januari 2026 katika saa za mcana kati.

Uongozi wa Chama AFC M23 unashutumu serkali ya Kinshasa kuwa ndio imesababisha shambulizi hayo alitangaza Lawrence Kanyuka  msemaji wa AFC M23 kwenye ukuta wake wa X.

Shambilizi hilo limetokea wakati mikataba ya Washington na DOHA iliomba pande mbili kisitisha mapigano na kuingiya kwenye meza ya mazungumzo, ila serkali ya Kinshasa ilisikika ikishutumu AFC M23 kuwa ndiye canzo ya kutoheshimu makubaliano hayo.

M23 kwa upande wake imeshutumu mara nyingi serkali ya Kinshasa kuensdesha baadhi ya shambulizi zidi ya ngome zake wilayani masisi na Rutshuru, hat ana kurusha bomu katikati mwa wakaaji.

Ni hapo tunafikia Mwisho wa matangazo yetu siku ya leo.

Msikilizaji hata mtazamaji ni kualike kuungana nasi katika habari zetu kwenye youtube, facebook na X ukiandika kivu news today TV; Mtangazo hay ana habari zingine yaendelea kwenye tuvuti yetu www.KIVUNEWSTODAY.COM

 Tukutane katika siku  zijazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Need Help?